Alhamisi, 28 Novemba 2024

Ijumaa ya mwisho November

Tags

Asalam alaykum uhali gani ndugu msomaji wa jukwaa hili. Nakukaribisha kwa mara nyengine tena tujumuike pamoja kwenye kupeana mitindi kuhusu mchakato mzima wa maisha yetu kwenda kutimiza kile ambacho Allah Taala amekiweka kwenye ndoto zetu. Ujumbe wangu Ijumaa ya leo ni kujifunga ipasavyo na sheria na miongozo yote ambavyotumetakiwa kuifuata kama Waislamu. Uislamu ni kujifunga na hukmu za kisheria na sivyenginevyo ndugu zangu. Bila kujifunga na hukmu za kisheria ipasavyo ikiwemo kuliweka la halali mahali pake na la haramu tukaliepuka kwa vile itakiwavyo. Basi uislamu wetu utakua na dosari kubwa na hatutofikia lengo la UchaMungu kama ilivyotakiwa. Ujumbe wangu kwako leo hii ni kujilazimisha kujifunga ipasavyo na hukmu za kisheria maishani mwako mwote katika kila kitendo ukitendacho. UchaMungu ni vitendo na wala si sio sifa. Ndugu yako. Suleiman Kh. Juma kwa mawasiliano: 0772800080/0656400761 karibuni sana tujifunze pamoja. Ijumaa Mubarak

This Is The Newest Post


EmoticonEmoticon