Karibu ndugu yangu na rafiki yangu kwa mara ya kwanza na kukaribisha katika mtandao huu ili tuweze kufahamishana juu ya umuhimu wa kuwa na ndoto ama malengo maishani mwetu ili tuweze kwa pamoja kufanikisha kile tulicho nacho hapa maishani.
Ukiwa ni mtu makini sana na mwenye kuyafikiria mambo utabaini kua uhai wetu tulio nao ndio rasilimali msingi kwetu basi kwa ivo sote kwa pamoja tunapaswa kuutumia kwa umakini kwa ajili ya kufanikisha malengo yetu kwa ufanisi yale tuliokua nayo.
Hivo ni jambo la muhimu kila mmoja wetu kuishi katika maisha haya kwa uangalifu na kwa nidhamu ya hali ya juu ili kwa uhai huu na umri mfupi tulio nao kuutumia vizuri ili siku tunayo ondoka katika ulimwengu isiwe ni siku ya majuto kwetu bali iwe ni siku ya furaha kwetu.
Ni kwa vipi ndugu msomaji mimi na wewe tutaweza kulifanikisha hilo ili maisha yetu tuyamalizie kwa furaha na kuondoka katika ulimwengu huu kuwa ni watu wa kupigiwa mfano kwa mafanikio na furaha tulio ondoka nayo. Jibu ni kwamba ni lazima tuwe na malengo katika maisha yetu kwani jambo lolote lile pasina kuwa na malengo madhubuti na makini jambo hlo litaishia kuambulia patupu lisilo na faida wala maana yoyote katika kutekelezwa kwake wala mafanikio yake.
Kuwa na malengo maishani ndio msingi utakao kuwezesha wewe kuishi maisha haya kwa mafanikio makubwa sana na kukuondeshea kila bugza ambayo kwako ingeli kugharimu na kukupotezea muda wako wote pasina kufikia jambo lolote lile unalo liwaza. Kwa maana hio ndugu yangu ni muhimu na ni muhimu zaidi ukalitambua hilo sasa na kuanza kulifanyia kazi leo kubaini na kuwa na uhakika katika maisha haya machache tulio nayo unapenda uwe nani au unapenda kufikia wapi.
Hivi ikiwa leo hii hapo ulipo kama Mungu atapenda akuongezee miaka 20 katika uhai wako hivi nini unatarajia utafanya katika umri wote huo na wapi unataka ufikie ili uweze kuimaliza hio miaka yako 20 uliopewa paka mwisho ukaimalizia kwa mafanikio makubwa na ukasema asante Mungu kwa kunipa maiaka hii 20. Kitu gani utafanya au utaishi tu ili mradi kwakua umepewa tu io miaka 20 kwaio ukawa kama wale wasio jijua wamepewa miaka mingapi katika maisha yao.kwani wao huishi alimradi wamalize siku tu katika umri wao.
Nnachotaka kukufahamisha hapa ni kwamba umri wako pasina malengo ni sawa na gari lisilo na dereva huwa linakwenda tu pasina kupishana na gari nyengine na kile kitakacho ikalia mbele yake ina gonga tu bila kizuizi chochote. Nataka nikwambie ndugu kuwa na malengo maishani na ukajua kile unachotakiwa kufanya kwa mujibu wa hayo matakwa ya malengo yako ndio msingi wa mafanikio ya uhai na maisha yako yote hapa duniani ili uweze kuishi maisha ya furaha yaliyojawa na neema tele.
Kama ndugu msomaji hadi hapo ulipo leo bado hujawa na lengo makhususi ama maalum katika kuyaendea maisha yako na kushauri leo bado hujachelewa ni vizuri sasa ukajipanga na kuangalia ni wapi unapotaka kwenda ili kumalizia kwa furaha maisha yako. Malengo yako ndio yatakayo kuwa somo kubwa kwa wale wote utakao waacha nyuma baada ya kukatika kwa na kumaliza kwa uhai wako.
Watu watakuhukumu aidha umefanikiwa au kuharibikiwa katika maisha yako ni kwa lile lengo tu ulilo nalo maishani mwako.
Jitambue sasa ili uwe ni mfano mzuri kwa jamii yako na kuacha athari kubwa kwa kizazi chako kwani utamfanya kila mmoja kuwa na hamu na shauku ya kuwa na mafanikio kama yako na wewe kuwa ni kigezo cha mafanikio kwa kizazi chako.
Siri kubwa ya kuwa na malengo maishani ni kukufanya kukitumia vizuri kipaji chako pamoja na rasilimali zako ulizonazo.ukiwa ni mtu unae ishi kwa malengo utaweza kuzitumia vizuri kabisa rasilimali zako zote ulizo nazo kwa nidhamu na mpangilio wa mzuri wa hali ya juu.
Utapata kuelewa kwa uwazi na kwa uwepesi kabisa ni njia gani ama ni hatua gani nizipite ili niweze kutumia kipaji change na rasilimali zangu chache nilizo nazo ili uweze kufikia mafanikio maishani mwako pasina kuharibu kipaji na rasilimali zako chache ulizonazo.
Kitu ambacho utaweza kukitumia kwa urahisi kabisa kujitambua na kupanga vizuri malengo yako ni kuangalia na kuchunguza kwa umakini zaidi ni vitu gani unapenda kusifiwa navyo kama utaweza kuwa navyo maishani mwako kwani ni lazima uwe na malengo yale yale tu uyapendayo maishani mwako.
Itazame sana akili yako ni kipi kizuri hukipa kipaombele katika kukiwaza na kukifikiria kwa muda mrefu kabisa kasha kutoa muangaza wa kukuahidi kama lau wewe utafikia hapa basi ni kweli utakua umefikia kileleni mwa mafanikio ya maisha yako.
Ni vizuri ukaanza kujitizama sasa ili kubaini ni wapi akili yako inakutuma ama inapendelea wewe uweze kukufikia ili uweze kuleta furaha na utulivu katika maisha yako na kukufanya uishi vile upendavyo katika maisha haya mafupi.
Haya yote na kusudia kukuzindua ndugu yangu kwani huwezi kufikia kabisa mafanikio yoyote yale uyajuayo pasina kuwa na malengo maishani mwako. Nnacho kushauri kwa mara nyengine tena ni lazima uhakikishe unapanga vizuri malengo yako ili uweze kufanikisha matarajio yote makubwa uliyo nayo maishani mwako.
Jipangie malengo yako sasa ili kuyapa muelekeo mzuri wa kimaendeleo na mafanikio makubwa maisha yako bila ya kupoteza chochote kile cha muhimu unacho kiwaza katika akili yako leo. Makala hii imeandikwa na Suleiman khamis (Jaula).
Kwa mawasiliano zaidi : +255772800080, +255656400761. E-mail: sulejaula@gmail.com, jaulasuleiman@gmail.com Tovuti yetu: www.jaulanetwork.blogspot.com
EmoticonEmoticon