Jumatatu, 16 Januari 2017

JAMBO MUHIMU LA KUZINGATIA WAKATI UNATAKA KUTIMIZA NDOTO ZAKO.





Habari yako na kukaribisha sana ndugu yangu mpenzi katika blog hii, kama lilivyo lengo kuu la kuanzishwa kwa blog hii ni kukuonyesha wewe na kukufunza ni namna gani ama ni njia zipi ambazo unaweza kuzipita ili kuweza kufanikisha malengo yako katika maisha haya. leo hii kwa ufupi kabisa nataka nikupe nukuu muhimu sana kutoka kwa mtu mmmoja maarufu sana aliepata mafanikio makubwa sana katika maisha yake.

Na nukuu yenyewe ni hii hapa “ A dream doesn’t become reality through magic. It takes sweaty, determination and hard work”. Haya ni maneno ya msingi kabisa na ni machache aliyoyasema Bwana Colin Powell. Inapaswa kuyaweka kwenye akili yako.

Maneno, haya yenye maana ya kwamba ndoto haiwezi kuwa ya kweli kama ni uchawi tu au kwa lugha nyengine tuseme kama ni miujiza tu imetokea au ni bahati mbaya  tu kutokea ni mfano kama umeamka asubuhi ukakuta mvua inanyesha. La hilo haliwezekani ata kidogo.

Lakini tukiendelea mbele na maneno haya yake yaliojawa na hekima na busara zisizo na kifani anasema kwamba ni lazima uchukue hatua ambazo zitakuwezesha uweze kufikia ama kuitimiza hio ndoto yako kwa mafanikio makubwa kabisa.

Kwanza kabisa lazima ikutoe jasho hapa ana maana gani, kilicho kusudiwa hapa ni kuwa ufanye juhudi za kivitendo kabisa ambazo ni hatua muhimu za kivitendo utakazo zifanya ili uweze kuyafikia malengo yako ambayo ndio hizo ndota zako maishani mwako.

Pili, lazima ufanye maamuzi tena yenye hekima na busara kabisa ni muhimu kuzingatia kwamba kama wewe unataka ufikie hatua ya kweli kutimiza ndoto zako ni lazima ifike wakati na uaamue kuwa sasa nitawacha kila nilicho nacho ambacho hakina kwangu mimi faida yoyote ila kunipotezea muda tu.Hii ni hatua muhimu kabisa kusema yaliopita tayari yameshapita na sasa nataka kufungua ukurasa mpya kabisa wa maisha yako ya sasa nay a baadae maamuzi yako utakayo yafanya hapa ndio itakua hatua muhimu kabisa kutekeleza ile hatua ya mwanzo tuliopita.

Muhimu na cha kuzingatia katika hatua hii ni kuanisha yale matarajio yako katika maisha yako na malengo yako kwa uwazi kabisa ni kitu gani unakusudia kukifikia ama una kilenga katika kufika ukomo wa maisha yako.

Ni lazima uamue hapa unataka kuwa nani na unataka kuwa na muelekeo gani katika maisha yako lakini pia hapa uamue unataka kumilika vitu gani kwa mujibu wa hayo malengo yako na matarajio yako uliyo ya kusudia maishani mwako.Katika kufanya maamuzi yako inakubidi ni lazima upime na kuichambua ndoto yako na uhalisia wako wa maisha yako, mazingira yako pamoja na fursa nyingi zilizo nazo unazo zijua na zile ambazo una lenga kuzijua ili kuweza kuyafikia malengo yako.

Fanya utafiti wa kutosha kwa kile unachotaka kukiamua lazima uwe na maarifa ya kutosha kwa hicho unacho taka kukifanyia maamuzi ili uweze kukijua vya kutosha. Kama ni biashara lazima ufanye utafiti wa kupata taarifa za kutosha kuhusiana na hio bidhaa yako pamoja na soko lake kwa wakati huo kwa ujumla.

Tafuta ushauri wa kutosha kwa watu mbali mbali khususan wale waliofanikiwa mnaofanana kwa hicho unachotaka kukifikia wewe. Unaweza kusoma vitabu vyao ama makala mbali mbali zinazohusiana na maisha yao au uchambuzi mzuri wa nadharia zao walizozitoa katika maisha yao.

Vizuri sana ukaamua leo ni vipi uantaka kuwa ili uweze kuianza safari yako mpya ya maisha yako yenye kulenga kufikia na kuzimiza ndoto zako kumbuka hakuna atakae kuja kukuamulia wala kukupangia jinsi gani ya kuamua bali ni wewe mwenyewe utekeleze hili jukumu lako la msingi.

Mwisho anasema ni lazima ufanye kazi ngumu akimaanisha ufanye kazi ya kweli kabisa na hapa unapaswa kujitolea kivilivyo kabisa wala sio kwa kubahatisha au kufanya mchezo na masihara katika hatua hii.
Lazima ufanye kazi ya kweli kabisa katika kufikia malengo yako na inakupasa kabisa kuutumia muda wako vizuri sana kwa nidhamu ya hali ya juu kwa kuhakikisha kila muda unaokufikia lazima ujue ni hatua gani unaipita ili kurahisisha kuyafikia malengo yako.

Fanya kazi kwa ari na bidii kubwa ili uweze kufanikisha malengo yako leo, chukua hatua hizi sasa ili uweze kufanikisha malengo yako leo amini kwa jitahada zako na maamuzi yako ndio nyenzo muhimu za kurahisisha safari yako ya kutimiza ndoto zako.

Tafadhali endelea kutembelea na kusoma makala nyenginezo muhimu kabisa zitakazo kuwezesha kutimiza kwa ufanisi ndoto zako maishani mwako. Zingatia haya leo na uyafanyie naamini utaona mabadiliko makubwa kwenye maisha yako.

                    Makala hii imeandikwa na Suleiman khamis  (Jaula).
           
                    Kwa mawasiliano zaidi : +255772800080, +255656400761.

                        E-mail: sulejaula@gmail.com,  jaulasuleiman@gmail.com

                                Tovuti yetu:   www.jaulanetwork.blogspot.com


EmoticonEmoticon