Jumatatu, 4 Novemba 2024

Nidhamu ndio msingi wa mafanikio

Tags

Ni ukweli usionashaka kuwa bila nidhamu juu ya msingi wa maisha yako yamafanikio huwezi kufanikiwa. Jambo lolote lile maishani linahitaji nidhamu ili liweze kupiga hatua moja kwenda nyengine. Vilevile mafanikio nayo yanahitaji nidhamu kubwa ili uweze kupiga hatua na kusema kuwa umefanikiwa. Nidhamu ni sheria au taratibu zinazofafanua juu ya kipi cha kufanya na kipi cha kuachana nacho kwa mujibu wa kile ulichokilenga kukifikia kwenye maisha yako. Malengo au Ndoto yako ndio itafafanua ni nidhamu ipi iwe ya fedha, muda au tabia uishike vipi ili iendene sambamba na kile unachokilenga. Huwezi kuwa na Ndoto za kuwa tajiri wakati ni mfujaji wa mali ma fedha zinazoingia kwako. kama vile huwezi kuwa na Ndoto za kuwa Mwanafunzi bora mwenye ufaulu mkubwa na mzuri kama huna nidhamu ya usomaji na muda wako vizuri unapokua Skuki au Chuoni. Hivyo kwa leo shika hili moja la kuwa na nidhamu kwenye mambo yako yote ili uweze kufanikiwa Ndugu yangu msomaji Mw. Suleiman Khamis Juma


EmoticonEmoticon