Vijana wengi wamekua wakihangaika kutafuta kipato cha kukidhi mahitaji yao ya kila siku pamoja na familia zao, jambo ambalo limekua likiwatia dhiki ya maisha na hadi kufikia wengine kukata tamaa juu ya jambo ilo. Lakini kwa mujibu wa taarifa, tafiti na ripoti za mashirika mbalimbali ulimwenguni yameeleza kuwa kwasasa huenda ujasiriamali ukawa ndio muarubaini wa tatizo hilo hususani kwa makundi ya wanawake na vijana. Hakunua nchi popote pale duniani yenye uwezo wa kuzalisha ajira za kutosha kwa wananchi wake iwe Serikalini ama Sekta binafsia zote pande hizo mbili haziwezi kutosheleza wananchi kupata ajira za kutosha kulingana na idadi kubwa ya watu iliopo sasa kote duniani. Lakini ni kitu kisichoshaka kuwa ujasiriamali ni fursa kubwa na pana yenye uwezo wa kutengeneza fursa nyingi kwa vijana ikiwemo kuwapa uwezo wa kijiajiri nahata wao wenyewe kuajiri vijana wenzao katika jamii zao. Hivyo kuweza kuweza kuziba pengo kubwa la idadi ya vijana wengi waliokosa ajira au kazi ndani ya nchi, uzalishaji kuongezeka na hivo kunyanyua kipato chao kwa kutimiza mahitaji yao lakini pia kuengeza pato la taifa kwa ujumla. Kwa mujibu wa ripoti ya vijana kwa mwaka 2020 ya ‘UN’ umoja wa mataifa iliotolewa tarehe 2 Julai 2020 yenye kichwa cha habari kisemacho “Ujasiriamali wa kijamii kwa vijana na ajenda 2030” imetoa wito kwa serikali na wadau wengine wafanyemaamuzi “kuondoa vikwazo kwa ujasiriamali kwa vijana kama vile fursa ya kupata mitaji ya kuanzia ambayo kwa sasa ni adimu na inawazuia vijana wengine kujihusisha katika shughuli mbalimbali zinazoweza kuwaletea faida.” Ripoti hii imetaja changamoto nyingi zinazowakumba wajasiriamali kama vile kukosa mitaji, masoko ya uhakikia na ugumu wa kupata mafunzo ya kutosha ya kuweza kuanzisha biashara na mengineo. Lakini pia haikusita pia kuonesha faida za ujasirimali katika makundi ya vijana na jamii kwa ujumla kama vile kutolea mifano watu wa jamii mbalimbali kwa jinsi gani wameanzisha shughuli za ujasiriamali katika jamii zao na kuweza kufanikiwa. Ujasiriliamali ni nini? Ripoti hiyo ya 2020 imeelezea ujasiriamali kama ni biashara ambayo inazalisha faida huku pia ikileta athari nzuri katika jamii. Ripoti inasema biashara za ujasiriliamali katika jamii zimewanufaisha watu milioni 871 katika kipindi cha miezi tisa tu kwenye nchi za Ulaya na Asia ya Kati mwaka 2016, kwa kutoa huduma na bidhaa zenye gharama ya takriban dola bilioni 6.7 na kuunda ajira hususan kwa makundi ya watu waliotengwa hasa vijana. Hakuna ukomo wa uanzishaji miradi ya ujasiriamali Ripoti hiyo imeweka bayana kwamba vijana wajasiriamali ambao tayari wameshaleta mabadiliko ni Pamoja na Zaid Souqi kutoka Jordan ambaye alianzisha ‘The Orenda Tribe” mwaka 2014 ambayo ni kazi ya Sanaa kwa ajili ya matumaini. Mradi wake wa Sanaa na mafunzo unawawezesha Watoto wa Syria na Jordan walio katika mazingira hatarishi. Mfano mwingine ni kutoka Malawi ambapo mkufunzi Ellen Chilemba alianzisha mradi wa Tiwale alipokuwa na umri wa miaka 18 na sasa ana miaka 30 mradi wake ni wa kuwapa mafunzo ya ujasiriamali wanawake, na hadi kufikia sasa wameshatoa mafunzo ya ujasiriamali wanawake 150. Chanzo https://news.un.org/sw/story/2020/07/1094212 Mifano hiyo na mengineo inatuonyesha wazi kuwa na sisi hata katika nchi zetu licha ya mazingira magumu tulionayo ya ukosefu wa mitaji na mengineo bado tunayo fursa ya kufanya shughuli za ujasiriamali ili kuwa ni njia ya kupata kipato chetu cha halali. Inahitaji kutumia vizuri vipawa tulivyonavyo pamoja na fursa zilizotuzunguka kupitia akili zetu na kuangalia namna gani tunaweza kufanikiwa kuanzisha miradi ya kijasiriamali japo midogo midogo ili iwe ni hatua ya mwanzo ya kuanzia kwa ajili ya kufikia malengo yetu. Penye nia pana njia hivyo lazima kila mmoja kuwa na malengo thabiti na yanayoshikika kwa dhamira ya dhati ya kutafuta wazo la biashara ambayo ataifanya kwa misingi ya kijasiriamali ili kuweza kujiajiri na kuweza kuwaajiri wengine pia. Kwa leo tutafikia hapa tukutane kwenye Makala nyengine, nikusihi usichoke kujifunza na kuendelea kufuatilia mafunzo mbalimbali kupitia blog yako hii. Makala hii imeandikwa na Suleiman Khamis Juma. Kwa mawasiliano zaidi : +255772800080, +255656400761. E-mail: sulejaula@gmail.com, Blog yetu: www.jaulanetwork.blogspot.com
Jumatatu, 18 Januari 2021
UJASIRIAMALI WAWEZA KUWA SULUHISHO LA KIPATO CHAKO

Tags
Artikel Terkait
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
EmoticonEmoticon