Ni jambo lililozoeleka katika jamii yetu kwa kila mmoja asikiapo neno biashara hupata taswira kubwa ndani ya kichwa chake kuwa ni kitu kikubwa kinachojumuisha mambo mengi rabda kama vile kuwa na pesa nyingi na vitu vingi vya aina mbalimbali vitakavyomuwezesha kufanya io biashara. Kitu hiki kimekua kikiwakwamisha watu wengi kuanza hata kitu kidogo ili kuchukua hatua ya kuanza kufanya biashara, jambo moja tusilo lijua ni kwamba kitu chochote kile tukitakacho kinataratibu na kanuni zake ambazo kupitia kanuni hizo ndio zitakazo amua je unaweza kuanza kufanya icho kitu au la. Tunapokuja katika suala la biashara nalo pia hubeba kanuni ambazo kila mmoja anapaswa kuzifuata kulingana na aina gani ya biashara anayotaka kuifanya kulingana na malengo na vipawa alivyonavyo ili kuweza kufanikiwa. Wataalamu mbalimbali waliofanya tafiti mbalimbali kuhusiana na biiashara na ujasiriamali wameelezea kanuni ama taratibu nyingi ambazo zote kwa pamoja unaweza kuzichukua ama baadhi yake ukaweza kuanzisha hio biashara yako. Jambo moja unalopaswa kufahamu nikua kitu chochote kile ukiacha biashara kinataka taaluma juu ya kitu hicho ni ngumu kuweza kufanikiwa kufanya kitu ama biashara na ukawuweza kufanikiwa kwenye kitu hicho pasina kuwa na uelewa japo wa ujumla kuhusu hicho kitu (general knowledge) itakayoweza kukuwezesha kukifanya icho kitu kama inavotakiwa. Watu wengi tumekua tukifeli kufanya vitu mbalimbali hasa biashara kutokana na ukosefu mkubwa wa ujuzi kutokana na hio biasahara tunayotaka kuifanya, kukurupuka na tamaa ya kupata fedha haraka ndio hututumbukiza kujiiingiza kufanya vitu pasina uelewa navyo. Hemu fikiria wewe mwenyewe binafsi kama utapewa gari uliendeshe na hujawahi kujifunza popote pale juu ya uendeshaji wa gari hiilo unafikiri kitu gani kitatokea zaidi ya kusababisha ajali kwa kuliharibu gari hilo lau kuwa utaweza angalau kuliondosha au kushindwa kuliondosha kabisa. Ujuzi ndio kitu pekee kitakacho kuwezesha kujua ni namna gani utaweza kuanza kufanya biashara yoyote ile uitakayo kuifanya kwakua tayari utajua moja kwa moja kitu gani unatakiwa uanze nacho na kipi kinafuata baada ya hatua io ya mwanzo. Ni ujuzi tu ndio pekee utakao kuwezesha kutoingia kwenye mitego ya kupoteza fedha zako kwa kujiingiza kwenye biashara katika mazingira hatarishi kwa biashara hio ulioichagua ambayo haiendani kufanyika katika eneo ilo kutokana na sababu mbalimbali mfano kukosekana kwa wateja wenye uhitaji wa bidhaa hio katika maeneo hayo. Hivyo ni jambo la msingi kwa yoyote yule mwenye ndoto na nia ya kuanza kufanya biashara ni muhimu kupata maarifa ya msingi juu ya hio biashara husika anayotaka kufanya ikiwa ni katika mifumo rasmini kama vile kwenda skuli au chuo kinachofundisha mafunzo ya biashara husika au mifumo isio rasmini kama kutembelea mitandao na kujisomea kibinafsi vitabu na matoleo mbalimbali yahusuyo biashara.
Na ndo mana sisi kwa kutambua umuhimu wa ilo tutakuwekea blog yetu hii rasmini kwa ajili ya kukusaidia kiurahisi kujifunza mambo mbalimbali yahusuyo biashara na ujasiriamali kwa urahisi sana pasina kutumia muda mrefu na fedha nyingi kuweza kupata ujuzi wowote ule unaoutaka. Hivyo usichoke kujifunza kwa chochote kile unachotaka kukifanya ili uweze kukifanya kwa ufanisi na kwa mafanikio ya hali ya juu kama vile unavotaka wewe mwenyewe. Kwa leo tutaishia hapa tukutane kwenye mfululizo wa kanuni nyengine ya kuanzisha biashara katika Makala ijayo ili uweze kujifunza vizuri mambo mengine yatakayokuwezesha kuanzisha biashara nzuri na yenye mafanikio makubwa na kuweza kukuingizia kipato chako. Makala hii imeandikwa na Suleiman Khamis Juma. Kwa mawasiliano zaidi : +255772800080, +255656400761. E-mail: sulejaula@gmail.com, Blog yetu: www.jaulanetwork.blogspot.comJumanne, 19 Januari 2021
KANUNI NDIO MSINGI MUHIMU WA KUANZISHA BIASHARA YOYOTE UITAKAYO - 01

Tags
Artikel Terkait
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
EmoticonEmoticon