Karibu kwa mara nyengine tena ndugu yangu msomaji katika blog hii, ikiwa leo tunaendelea na mada yetu kama ilivyo kwenye kichwa cha habari kanuni ndio msingi muhimu wa kuanzisha biashara yoyote uitakayo . Jana tulianza kwa kuangalia kanuni ya kwanza ambayo ilikua ni kupata mafunzo kabla japo kwa jumla tu kuhusiana na biashara unayotaka kufanya kitu ambacho tuliona kwa kiasi kikubwa kinaweza kukuepusha na hatari nyingi ikiwemo kupoteza fedha kwakufanya uwekezaji kwenye biashara ama sehemu isiofaa. Ni kusihi tu kama bado hujaisoma ile Makala ya mwanzo ya mada hii ni vizuri ukarudi mwanzo kwenye blog hii ili uweze kuisoma Makala hio na ndipo baadae urudi kuendelea kuisoma Makala hii ya pili ili uweze kupata msingi mzuri wa maarifa katika hichi tunachoendelea kukizungumza. Kwa siku ya leo tukiendelea na somo letu tutaangali mataarisho hii huweza kuifanya kuwa ni hatua yako ya pili mara baada kupata mafunzo na kuamua hio biashara unayotaka kufanya, tayari umeshajua nini biashara na kipi kinahitajika kufanywa katika biashara. Sasa kabla ya yote lile ni lazima ufanye mataarisho ya kutosha kutokana na aina ya biashara uliokusudia kufanya, mataarisho huenda ikawa ni kutafuta mtaji au sehemu nzuri yenye mazingira ya kuvutia kwa ajili ya biashara yako. Kumbuka pasina mataarisho mazuri nay a kutosha basi ni kujiandaa kufeli kwa biashara yako, tukumbuke msemo maarufu sana usemao “usipojiandaa kwa ushindi basi unajiandaa kushindwa” Kutokana na msemo huo haitaki kuwa na elimu kubwa sana kujua kwamba mataarisho juu ya jambo lolote lile ni kitu cha msingi na muhimu kwa kufanikiwa ama kufeli kwa jambo husika. Ni mataarisho tu ndiyo yatakayo amua hatma kubwa ama kufika mbali kwa biashara yako kwani wakati unapofanya mataarisho ndipo utapoweza kubaini kipi na kipi unatakiwa kufanya ili biashara yako iweze kukua kwa haraka zaidi. Na isitoshe ndipo pia utapoweza kujua ni kipi na kipi ujiepushe nacho kwa kuhofia kuharibu biashara yako, watu wengi wameingia kwenye mtego wakupoteza biashara zao kutokana na mataarisho mabovu ama madogo wakati wakati wakitaka kuanzisha biashara zao. Mataarisho ya mwanzo kabisa unayotakiwa kuyafanya mara tu unapotaka kuanzisha biashara yako ni kuhakikisha una mtaji wa kutosha wa kuanzisha biashara husika, na hapa ieleweke tunapozungumza mtaji haimaanishi kama uwe na kiasi kikubwa sana cha fedha bali ni kile kiasi tu cha kuweza kununua malighafi zitakiwazo kwa mara ya kwanza kuweza kufanya uzalishaji wa bidhaa husika kama unataka kufanya biashara ya uzalishaji kama vile kutengeneza sabuni. Hii ni ile fedha itakayokuwezesha kupata mahitaji muhimu ya kuanzia katika biashara husika ulioamua kuifanya kulingana na mahitaji yake kitaalam, kwani kila biashara hutofautiana na biashara nyengine kwenye vitu vinavyohitajika kuanzisha biashara hio. Eneo au mahali pakufanyia baishara yako ni lazima liwe eneo zuri na lenye kufaa kwa biashara hio unayotaka kuifanya, sio kila sehemu unaweza kufanya kila biashara kwa hivo ni lazima uangalie ni maeneo sahihi kwa aina hio ya biashara uliokusudia kufanya, tutakuja kulielezea na kulifafanua vizuri zaidi hili wakati tutakapo kuja kuzungumzia kanuni ya kuchagua soko ama eneo la kufanyia biashara yako. Yako mambo mengi mengi ambayo unatakiwa kuyafanyia mataarisho kabla ya kuanza kufanya biashara yoyote ile ili uweze kupata faida ilio kusudiwa lakini tutayaeleza kwa mtiririko mzuri na kwa ufafanuzi katika muendelezo wa mada hii katika Makala zijazo ili tuweze kujifunza kidogo kidogo na kupata faida iliokusudiwa. Makala hii imeandikwa na Suleiman Khamis Juma. Kwa mawasiliano zaidi : +255772800080, +255656400761. E-mail: sulejaula@gmail.com, Blog yetu: jaulanetwork.blogspot.com
Jumatano, 20 Januari 2021
KANUNI NDIO MSINGI MUHIMU WA KUANZISHA BIASHARA YOYOTE UITAKAYO – 02

Tags
Artikel Terkait
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
EmoticonEmoticon