Jumatatu, 25 Januari 2021

KANUNI NDIO MSINGI MUHIMU WA KUANZISHA BIASHARA YOYOTE UITAKAYO – 03

Tags

Karibu kwa mara nyengine tena ndugu yangu kwa ajili ya kuendelea kujifunza somo muhimu la kanuni za biashara ili uweze kuanzisha ama kuendesha biashara yako kwa ufanisi na kupata matokeo makubwa unayoyataka. Jana tuliishia kwa kuangalia kanuni ya pili isemayo mataarisho kabla ya kuanza biashara kama tulivoona sote kwa pamoja kuwa jambo lolote lile maishani kabla ya hatua ya mwanzo kuanza kulifanya unahitajika kufanya mataarisho. Tulizungumza na kuona kivitendo kabisa kuwa mataarisho ndio yatakayo amu hatma ya biashara io kama itafika mbali au itaishia njiani na kama je inaweza kupata mafanikio au la. Hayo maswali yote yatajibiwa kutokana na mataaarisho ulioyafanya kama uliyafanya vizuri kwa kutimiza yale yote yaliotakiwa ili biashara yako ianze vizuri. Ama ulikurupuka kutokana na mihemko ya kutaka faida za haraka na tahamaki yake ukaja ukajikuta unakula hasara kwa kupoteza mtaji pamoja na rasilimali zako zote na usione faida yoyote kwenye biashara ile uliojiingiza kuifanya. Leo tutaendele na kipengele hikihiki cha kufanya mataarisho kabla ya kufanya biashara kutokana na umuhimu wake mkubwa na matokeo yake unayoweza kuyapata ili kufanya biashara yako kwa mafanikio makubwa sana. Utafiti ni kitu muhimu sana katika mataarisho ya kufanya jambo lolote lile ni lazima ufanye utafiti wa kutosha kuhusu jambo husika kama kweli utaweza kumudu kulifanya au la je utaweza kulifanya katika mazingira gani na ukaweza kufanikiwa. Kutafiti ni kwa njia zipi utaweza kupata kwa urahisi bidhaa unazotaka kuuza, utazitolea wapi na kwa njia gani ?, na hio njia je ? gharama yake ni kiasi gani ? wewe mwenyewe gharama io utaiweza na kivipi ? Wateja wako ni akina nani ? kumbuka sio kila mtu anaweza kuwa mteja wako hivo ni lazima kabla ya chochote uwe tayari umeshafanya utafiti wa kujiridhisha kabisa kujua ni aina gani ya wateja unaowataka ili uweze kuwapelekea bidhaa zako. Baada ya kujua hao wateja wako ni lazima pia ujue utawapata wapi au bidhaa zako utawafikishia kwa njia gani na je hio njia kweli ni muafaka kwa wateja wa aina hio kupata bidhaa hizo haitokuja kuwa ni kikwazo kwako au wao kufikiwa na bidhaa zako. Tabia zao zikoje hao wateja uliowalenga, wanapenda bidhaa kama hio kwa urahisi au la na vipi kwa izo gharama ulizozipata kwa kuuza kwa bei ya gharama io wao wataweza kuimudu kweli au itawashinda. Na hapa ndo unakuja kutafiti tena na ambako ni muhimu ni kuhusu bei ya kuuzia hio biashara yako wakati tayari umeshatoa gharama zako zote ni lazima upangilie vizuri bei ya bidhaa zako, usije kukurupuka tu ukaweka bei kiholela mwishowe ukajikuta unakula hasara kutokana na bei hio.

Pengine ultumia gharama kubwa sana kuweza kuizalisha bidhaa yako hio ama gharama za usafirishaji wake kutoka sehemu ulioipata hadi sehemu ya kuuzia. Kwa leo tutaishia hapa tukutake kwenye kanuni nyengine miongoni mwa kanuni muhimu za kuanzisha ama kuendeleza biashara yoyote ile na ukaweza kupata mafanikio makubwa kama vile ulivyokusudia. Makala hii imeandikwa na Suleiman Khamis Juma. Kwa mawasiliano zaidi : +255772800080, +255656400761. E-mail: sulejaula@gmail.com, Blog yetu: jaulanetwork.blogspot.com


EmoticonEmoticon