Asalam alaykum
uhali gani ndugu msomaji wa jukwaa hili. Nakukaribisha kwa mara nyengine tena tujumuike pamoja kwenye kupeana mitindi kuhusu mchakato mzima wa maisha yetu kwenda kutimiza kile ambacho Allah Taala amekiweka kwenye ndoto zetu.
Ujumbe wangu Ijumaa ya leo ni kujifunga ipasavyo na sheria na miongozo yote ambavyotumetakiwa kuifuata kama Waislamu. Uislamu ni kujifunga na hukmu za kisheria na sivyenginevyo ndugu zangu.
Bila kujifunga na hukmu za kisheria ipasavyo ikiwemo kuliweka la halali mahali pake na la haramu tukaliepuka kwa vile itakiwavyo. Basi uislamu wetu utakua na dosari kubwa na hatutofikia lengo la UchaMungu kama ilivyotakiwa.
Ujumbe wangu kwako leo hii ni kujilazimisha kujifunga ipasavyo na hukmu za kisheria maishani mwako mwote katika kila kitendo ukitendacho. UchaMungu ni vitendo na wala si sio sifa.
Ndugu yako. Suleiman Kh. Juma
kwa mawasiliano:
0772800080/0656400761
karibuni sana tujifunze pamoja.
Ijumaa Mubarak
Alhamisi, 28 Novemba 2024
Jumanne, 12 Novemba 2024
Jumatatu, 4 Novemba 2024
Nidhamu ndio msingi wa mafanikio
Ni ukweli usionashaka kuwa bila nidhamu juu ya msingi wa maisha yako yamafanikio huwezi kufanikiwa. Jambo lolote lile maishani linahitaji nidhamu ili liweze kupiga hatua moja kwenda nyengine. Vilevile mafanikio nayo yanahitaji nidhamu kubwa ili uweze kupiga hatua na kusema kuwa umefanikiwa.
Nidhamu ni sheria au taratibu zinazofafanua juu ya kipi cha kufanya na kipi cha kuachana nacho kwa mujibu wa kile ulichokilenga kukifikia kwenye maisha yako.
Malengo au Ndoto yako ndio itafafanua ni nidhamu ipi iwe ya fedha, muda au tabia uishike vipi ili iendene sambamba na kile unachokilenga.
Huwezi kuwa na Ndoto za kuwa tajiri wakati ni mfujaji wa mali ma fedha zinazoingia kwako. kama vile huwezi kuwa na Ndoto za kuwa Mwanafunzi bora mwenye ufaulu mkubwa na mzuri kama huna nidhamu ya usomaji na muda wako vizuri unapokua Skuki au Chuoni.
Hivyo kwa leo shika hili moja la kuwa na nidhamu kwenye mambo yako yote ili uweze kufanikiwa Ndugu yangu msomaji
Mw. Suleiman Khamis Juma
Jumamosi, 3 Agosti 2024
TAARIFA MPYA
Asalam alaykum Habarani ndugu zangu, natumai muwazima wa afya mara baada ukimya
wa muda mrefu kwa taarifa hii ni kuwa muda simrefu tutarudi hewani tena katika
jukwaa hili lengo ikiwa ni kuendelea na mafunzo yetu kwa pale tulipoishia.
karibuni sana kwa mara nyengine tena mupate kujifunza kama tulivyokua awali.
karibuni sana
Jumatatu, 25 Januari 2021
KANUNI NDIO MSINGI MUHIMU WA KUANZISHA BIASHARA YOYOTE UITAKAYO – 03
Karibu kwa mara nyengine tena ndugu yangu kwa ajili ya kuendelea kujifunza somo muhimu la kanuni za biashara ili uweze kuanzisha ama kuendesha biashara yako kwa ufanisi na kupata matokeo makubwa unayoyataka.
Jana tuliishia kwa kuangalia kanuni ya pili isemayo mataarisho kabla ya kuanza biashara kama tulivoona sote kwa pamoja kuwa jambo lolote lile maishani kabla ya hatua ya mwanzo kuanza kulifanya unahitajika kufanya mataarisho.
Tulizungumza na kuona kivitendo kabisa kuwa mataarisho ndio yatakayo amu hatma ya biashara io kama itafika mbali au itaishia njiani na kama je inaweza kupata mafanikio au la. Hayo maswali yote yatajibiwa kutokana na mataaarisho ulioyafanya kama uliyafanya vizuri kwa kutimiza yale yote yaliotakiwa ili biashara yako ianze vizuri.
Ama ulikurupuka kutokana na mihemko ya kutaka faida za haraka na tahamaki yake ukaja ukajikuta unakula hasara kwa kupoteza mtaji pamoja na rasilimali zako zote na usione faida yoyote kwenye biashara ile uliojiingiza kuifanya.
Leo tutaendele na kipengele hikihiki cha kufanya mataarisho kabla ya kufanya biashara kutokana na umuhimu wake mkubwa na matokeo yake unayoweza kuyapata ili kufanya biashara yako kwa mafanikio makubwa sana.
Utafiti ni kitu muhimu sana katika mataarisho ya kufanya jambo lolote lile ni lazima ufanye utafiti wa kutosha kuhusu jambo husika kama kweli utaweza kumudu kulifanya au la je utaweza kulifanya katika mazingira gani na ukaweza kufanikiwa.
Kutafiti ni kwa njia zipi utaweza kupata kwa urahisi bidhaa unazotaka kuuza, utazitolea wapi na kwa njia gani ?, na hio njia je ? gharama yake ni kiasi gani ? wewe mwenyewe gharama io utaiweza na kivipi ?
Wateja wako ni akina nani ? kumbuka sio kila mtu anaweza kuwa mteja wako hivo ni lazima kabla ya chochote uwe tayari umeshafanya utafiti wa kujiridhisha kabisa kujua ni aina gani ya wateja unaowataka ili uweze kuwapelekea bidhaa zako.
Baada ya kujua hao wateja wako ni lazima pia ujue utawapata wapi au bidhaa zako utawafikishia kwa njia gani na je hio njia kweli ni muafaka kwa wateja wa aina hio kupata bidhaa hizo haitokuja kuwa ni kikwazo kwako au wao kufikiwa na bidhaa zako.
Tabia zao zikoje hao wateja uliowalenga, wanapenda bidhaa kama hio kwa urahisi au la na vipi kwa izo gharama ulizozipata kwa kuuza kwa bei ya gharama io wao wataweza kuimudu kweli au itawashinda.
Na hapa ndo unakuja kutafiti tena na ambako ni muhimu ni kuhusu bei ya kuuzia hio biashara yako wakati tayari umeshatoa gharama zako zote ni lazima upangilie vizuri bei ya bidhaa zako, usije kukurupuka tu ukaweka bei kiholela mwishowe ukajikuta unakula hasara kutokana na bei hio.
Pengine ultumia gharama kubwa sana kuweza kuizalisha bidhaa yako hio ama gharama za usafirishaji wake kutoka sehemu ulioipata hadi sehemu ya kuuzia.
Kwa leo tutaishia hapa tukutake kwenye kanuni nyengine miongoni mwa kanuni muhimu za kuanzisha ama kuendeleza biashara yoyote ile na ukaweza kupata mafanikio makubwa kama vile ulivyokusudia.
Makala hii imeandikwa na Suleiman Khamis Juma.
Kwa mawasiliano zaidi : +255772800080, +255656400761.
E-mail: sulejaula@gmail.com, Blog yetu: jaulanetwork.blogspot.com
Jumatano, 20 Januari 2021
KANUNI NDIO MSINGI MUHIMU WA KUANZISHA BIASHARA YOYOTE UITAKAYO – 02
Karibu kwa mara nyengine tena ndugu yangu msomaji katika blog hii, ikiwa leo tunaendelea na mada yetu kama ilivyo kwenye kichwa cha habari kanuni ndio msingi muhimu wa kuanzisha biashara yoyote uitakayo .
Jana tulianza kwa kuangalia kanuni ya kwanza ambayo ilikua ni kupata mafunzo kabla japo kwa jumla tu kuhusiana na biashara unayotaka kufanya kitu ambacho tuliona kwa kiasi kikubwa kinaweza kukuepusha na hatari nyingi ikiwemo kupoteza fedha kwakufanya uwekezaji kwenye biashara ama sehemu isiofaa.
Ni kusihi tu kama bado hujaisoma ile Makala ya mwanzo ya mada hii ni vizuri ukarudi mwanzo kwenye blog hii ili uweze kuisoma Makala hio na ndipo baadae urudi kuendelea kuisoma Makala hii ya pili ili uweze kupata msingi mzuri wa maarifa katika hichi tunachoendelea kukizungumza.
Kwa siku ya leo tukiendelea na somo letu tutaangali mataarisho hii huweza kuifanya kuwa ni hatua yako ya pili mara baada kupata mafunzo na kuamua hio biashara unayotaka kufanya, tayari umeshajua nini biashara na kipi kinahitajika kufanywa katika biashara.
Sasa kabla ya yote lile ni lazima ufanye mataarisho ya kutosha kutokana na aina ya biashara uliokusudia kufanya, mataarisho huenda ikawa ni kutafuta mtaji au sehemu nzuri yenye mazingira ya kuvutia kwa ajili ya biashara yako.
Kumbuka pasina mataarisho mazuri nay a kutosha basi ni kujiandaa kufeli kwa biashara yako, tukumbuke msemo maarufu sana usemao “usipojiandaa kwa ushindi basi unajiandaa kushindwa”
Kutokana na msemo huo haitaki kuwa na elimu kubwa sana kujua kwamba mataarisho juu ya jambo lolote lile ni kitu cha msingi na muhimu kwa kufanikiwa ama kufeli kwa jambo husika.
Ni mataarisho tu ndiyo yatakayo amua hatma kubwa ama kufika mbali kwa biashara yako kwani wakati unapofanya mataarisho ndipo utapoweza kubaini kipi na kipi unatakiwa kufanya ili biashara yako iweze kukua kwa haraka zaidi.
Na isitoshe ndipo pia utapoweza kujua ni kipi na kipi ujiepushe nacho kwa kuhofia kuharibu biashara yako, watu wengi wameingia kwenye mtego wakupoteza biashara zao kutokana na mataarisho mabovu ama madogo wakati wakati wakitaka kuanzisha biashara zao.
Mataarisho ya mwanzo kabisa unayotakiwa kuyafanya mara tu unapotaka kuanzisha biashara yako ni kuhakikisha una mtaji wa kutosha wa kuanzisha biashara husika, na hapa ieleweke tunapozungumza mtaji haimaanishi kama uwe na kiasi kikubwa sana cha fedha bali ni kile kiasi tu cha kuweza kununua malighafi zitakiwazo kwa mara ya kwanza kuweza kufanya uzalishaji wa bidhaa husika kama unataka kufanya biashara ya uzalishaji kama vile kutengeneza sabuni.
Hii ni ile fedha itakayokuwezesha kupata mahitaji muhimu ya kuanzia katika biashara husika ulioamua kuifanya kulingana na mahitaji yake kitaalam, kwani kila biashara hutofautiana na biashara nyengine kwenye vitu vinavyohitajika kuanzisha biashara hio.
Eneo au mahali pakufanyia baishara yako ni lazima liwe eneo zuri na lenye kufaa kwa biashara hio unayotaka kuifanya, sio kila sehemu unaweza kufanya kila biashara kwa hivo ni lazima uangalie ni maeneo sahihi kwa aina hio ya biashara uliokusudia kufanya, tutakuja kulielezea na kulifafanua vizuri zaidi hili wakati tutakapo kuja kuzungumzia kanuni ya kuchagua soko ama eneo la kufanyia biashara yako.
Yako mambo mengi mengi ambayo unatakiwa kuyafanyia mataarisho kabla ya kuanza kufanya biashara yoyote ile ili uweze kupata faida ilio kusudiwa lakini tutayaeleza kwa mtiririko mzuri na kwa ufafanuzi katika muendelezo wa mada hii katika Makala zijazo ili tuweze kujifunza kidogo kidogo na kupata faida iliokusudiwa.
Makala hii imeandikwa na Suleiman Khamis Juma.
Kwa mawasiliano zaidi : +255772800080, +255656400761.
E-mail: sulejaula@gmail.com, Blog yetu: jaulanetwork.blogspot.com
Jumanne, 19 Januari 2021
KANUNI NDIO MSINGI MUHIMU WA KUANZISHA BIASHARA YOYOTE UITAKAYO - 01
Ni jambo lililozoeleka katika jamii yetu kwa kila mmoja asikiapo neno biashara hupata taswira kubwa ndani ya kichwa chake kuwa ni kitu kikubwa kinachojumuisha mambo mengi rabda kama vile kuwa na pesa nyingi na vitu vingi vya aina mbalimbali vitakavyomuwezesha kufanya io biashara.
Kitu hiki kimekua kikiwakwamisha watu wengi kuanza hata kitu kidogo ili kuchukua hatua ya kuanza kufanya biashara, jambo moja tusilo lijua ni kwamba kitu chochote kile tukitakacho kinataratibu na kanuni zake ambazo kupitia kanuni hizo ndio zitakazo amua je unaweza kuanza kufanya icho kitu au la.
Tunapokuja katika suala la biashara nalo pia hubeba kanuni ambazo kila mmoja anapaswa kuzifuata kulingana na aina gani ya biashara anayotaka kuifanya kulingana na malengo na vipawa alivyonavyo ili kuweza kufanikiwa.
Wataalamu mbalimbali waliofanya tafiti mbalimbali kuhusiana na biiashara na ujasiriamali wameelezea kanuni ama taratibu nyingi ambazo zote kwa pamoja unaweza kuzichukua ama baadhi yake ukaweza kuanzisha hio biashara yako.
Jambo moja unalopaswa kufahamu nikua kitu chochote kile ukiacha biashara kinataka taaluma juu ya kitu hicho ni ngumu kuweza kufanikiwa kufanya kitu ama biashara na ukawuweza kufanikiwa kwenye kitu hicho pasina kuwa na uelewa japo wa ujumla kuhusu hicho kitu (general knowledge) itakayoweza kukuwezesha kukifanya icho kitu kama inavotakiwa.
Watu wengi tumekua tukifeli kufanya vitu mbalimbali hasa biashara kutokana na ukosefu mkubwa wa ujuzi kutokana na hio biasahara tunayotaka kuifanya, kukurupuka na tamaa ya kupata fedha haraka ndio hututumbukiza kujiiingiza kufanya vitu pasina uelewa navyo.
Hemu fikiria wewe mwenyewe binafsi kama utapewa gari uliendeshe na hujawahi kujifunza popote pale juu ya uendeshaji wa gari hiilo unafikiri kitu gani kitatokea zaidi ya kusababisha ajali kwa kuliharibu gari hilo lau kuwa utaweza angalau kuliondosha au kushindwa kuliondosha kabisa.
Ujuzi ndio kitu pekee kitakacho kuwezesha kujua ni namna gani utaweza kuanza kufanya biashara yoyote ile uitakayo kuifanya kwakua tayari utajua moja kwa moja kitu gani unatakiwa uanze nacho na kipi kinafuata baada ya hatua io ya mwanzo.
Ni ujuzi tu ndio pekee utakao kuwezesha kutoingia kwenye mitego ya kupoteza fedha zako kwa kujiingiza kwenye biashara katika mazingira hatarishi kwa biashara hio ulioichagua ambayo haiendani kufanyika katika eneo ilo kutokana na sababu mbalimbali mfano kukosekana kwa wateja wenye uhitaji wa bidhaa hio katika maeneo hayo.
Hivyo ni jambo la msingi kwa yoyote yule mwenye ndoto na nia ya kuanza kufanya biashara ni muhimu kupata maarifa ya msingi juu ya hio biashara husika anayotaka kufanya ikiwa ni katika mifumo rasmini kama vile kwenda skuli au chuo kinachofundisha mafunzo ya biashara husika au mifumo isio rasmini kama kutembelea mitandao na kujisomea kibinafsi vitabu na matoleo mbalimbali yahusuyo biashara.
Na ndo mana sisi kwa kutambua umuhimu wa ilo tutakuwekea blog yetu hii rasmini kwa ajili ya kukusaidia kiurahisi kujifunza mambo mbalimbali yahusuyo biashara na ujasiriamali kwa urahisi sana pasina kutumia muda mrefu na fedha nyingi kuweza kupata ujuzi wowote ule unaoutaka.
Hivyo usichoke kujifunza kwa chochote kile unachotaka kukifanya ili uweze kukifanya kwa ufanisi na kwa mafanikio ya hali ya juu kama vile unavotaka wewe mwenyewe.
Kwa leo tutaishia hapa tukutane kwenye mfululizo wa kanuni nyengine ya kuanzisha biashara katika Makala ijayo ili uweze kujifunza vizuri mambo mengine yatakayokuwezesha kuanzisha biashara nzuri na yenye mafanikio makubwa na kuweza kukuingizia kipato chako.
Makala hii imeandikwa na Suleiman Khamis Juma.
Kwa mawasiliano zaidi : +255772800080, +255656400761.
E-mail: sulejaula@gmail.com, Blog yetu: www.jaulanetwork.blogspot.com
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)